WAJIBU, kwa kushirikiana na Twaweza East Africa na PPRA, kwa msaada wa Open Contracting Partnership, imetekeleza mradi wa kuboresha ushiriki wa wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) na makundi maalum katika ununuzi wa umma kupitia mfumo wa NeST. Mradi ulifanyika katika halmashauri tano, ikiwemo Igunga na Sikonge mkoani Tabora. SMEs 447 zilipatiwa mafunzo (wanawake 166, wanaume 281), na usajili kwenye NeST uliongezeka kwa zaidi ya asilimia 25. Kati ya wafanyabiashara 60 waliotuma maombi ya zabuni, 38 walishinda. Mfanyabiashara wa matofali kutoka Igunga alishinda zabuni ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Migerere, na Halmashauri ya Igunga inasema wazabuni wa ndani wakiwa wengi, fedha zinabaki kwenye jamii.
|
TABORA IGUNGA NEST Kuimarisha Ushiriki wa Wafanyabiashara Wadogo kupitia Mfumo wa NeST |
|||||||||
|
WAJIBU, kwa kushirikiana na Twaweza East Africa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kwa msaada wa Open Contracting Partnership (OCP), imetekeleza mradi wenye lengo la kuboresha ushiriki wa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SMEs) na makundi maalum katika mchakato wa ununuzi wa umma kwa kutumia mfumo wa NeST. Mradi huu umetekelezwa katika Halmashauri tano: Wilaya ya Igunga na Sikonge mkoani Tabora, Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, na Halmashauri ya Jiji la Mbeya. |
|
||||||||
|
447 Kwa ujumla, SMEs zilipatiwa mafunzo |
166 Wanawake |
281 Wanaume |
25% Baada ya mafunzo, kulikuwa na ongezeko la zaidi ya asilimia 25 za usajili wa biashara katika mfumo wa NeST. |
||||||
|
Aidha, kati ya wafanyabiashara 60 waliotuma maombi ya zabuni, 38 waliweza kushinda, wengine zaidi ya mara mbili. Katika Wilaya ya Igunga pekee, zaidi ya wafanyabiashara wadogo 100 walinufaika na mafunzo haya. Vilevile, wafanyabiashara waliongeza uelewa wao kuhusu utaratibu wa zabuni za serikali, jambo lililowasaidia kujisajili na kushiriki kwa ufanisi zaidi. |
|||||||||
|
|
Mmoja wa wanufaika wa mafunzo haya alieleza: “Mafunzo ya WAJIBU yametusaidia sana. Awali hatukujua namna ya kushiriki katika ununuzi wa umma, lakini baada ya mafunzo haya, nimeweza kushinda zabuni zaidi ya moja kupitia mfumo wa NeST.” Wafanyabiashara wengine walisema mfumo huu umekuwa mkombozi kwao, kwani awali walikuwa na changamoto za kutambua hatua sahihi za kushiriki katika mchakato wa ununuzi wa umma. |
||||||||
|
|
Mfanyabiashara mmoja wa matofali kutoka Igunga alieleza kuwa aliweza kushinda zabuni ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Migerere, Wilaya ya Igunga. Alieleza kuwa mfumo wa NeST umemwezesha kuomba zabuni zaidi ya moja na kushinda kwa uwazi na haki. “Nimeweza kupata zabuni kupitia NeST, na sasa biashara yangu imeimarika zaidi,” alisema mfanyabiashara huyo. |
||||||||
|
Halmashauri ya Igunga imeripoti kuwa mfumo wa NeST umeongeza idadi ya wazabuni wa ndani wanaoshiriki katika mchakato wa ununuzi wa umma. “Tunapokuwa na wazabuni wengi wa ndani, fedha zinabaki kwenye jamii yetu, tofauti na awali ambapo fursa nyingi zilichukuliwa na wazabuni kutoka maeneo mengine kupitia mfumo wa zamani wa TANEPS,” alisema Afisa Ununuzi Halmashauri ya Igunga. |
|||||||||
|
Wito umetolewa kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kujiunga na mfumo wa NeST ili waweze kushiriki katika zabuni za serikali. Sheria ya manunuzi ya umma namba 10 inataka zabuni zote zifanyike kupitia mfumo wa kidigitali, hivyo ni muhimu kwa wafanyabiashara kuwa sehemu ya mabadiliko haya. |
|||||||||
|
|
Jifunze zaidi |
|
|||||||

.png&w=1920&fm=webp&q=72)

